Home » , » JALADA LA KESI YA LULU MICHAEL LAPELEKWA KISUTU

JALADA LA KESI YA LULU MICHAEL LAPELEKWA KISUTU

Written By JUMA MPEKUZI on Tuesday, October 23, 2012 | 5:39:00 AMMSANII  wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji, amehoji Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu lilikofikia jalada la kesi.

Lulu aliuliza swali hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Stuarti Sanga baada ya Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao kudai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba, upelelezi wake haujakamilika.

Baada ya Sekwao kueleza hiyo, Lulu alinyoosha mkono na kuhoji jalada la kesi inayomkabili lilikofikia.

Hakimu Sanga alimuuliza Wakili Sekwao iwapo anauliza jalada halisi au la kudurufu. 

Wakili Sekwao alimwambia Hakimu Sanga kuwa, anaulizia jalada halisi.Hakimu Sanga alimwambia Lulu kuwa jalada halisi limekwisharudi  na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 5, mwaka huu itakapotajwa tena.

Lulu anatuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba. Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwa Kanumba, Sinza, Dar es Salaam.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts