Home » , , » "NIMECHOKA KUTAPELIWA KIMAPENZI NA SIHITAJI KULIA TENA"....JACK WOLPER

"NIMECHOKA KUTAPELIWA KIMAPENZI NA SIHITAJI KULIA TENA"....JACK WOLPER

Written By JUMA MPEKUZI on Wednesday, October 31, 2012 | 7:58:00 AMWapambe kadhaa wa msanii Jackline Wolper wamelonga na mwandishi wetu  kuwa, hivi sasa Wolper haitaji kulia tena kwenye mapenzi hivyo amepanga mwanaume ambaye atamtangaza muda wowote basi watu wajue kuwa ndiye mume kabisa kwani haitaji tena kuumizwa.

Wapambe hao ambao mara nyingi huwa karibu na msanii huyo, walifunguka kuwa kwa sasa msanii huyo hana mwanaume na endapo akimpata basi ataamua kufanya hivyo ili kuzuia matatizo mengine yanayoweza kutokea kama kuibiwa na watoto wenyewe njaa kali wanajifanya wamesomea mapenzi.


Hata hivyo walidai kuwa kingine ambacho msanii huyo hataki kukosea tena ni kumtangaza mpenzi wake kwa mademu wa bongo movie kwani wanahusika mara kadhaa kwa kuharibu mapenzi yake kwani hawakawii kufanya mapinduzi.


“Ishu iko hivyo mjini hapa kila mtu ana mipango lakini kwa upande wa mwanadada Wolper mambo yako hivyo na hataki kupoteza muda kwa sababu mademu wa tasnia hiyo wana tabia ya kumzoea mtu kwa dakika kadhaa baada ya hapo kwisha habari wanaondoka mwanaume kama hawana akili nzuri,”
alisema mpambe.

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimtafuta
Wolper ili kutoa la moyoni naye alidai kuwa lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja hivyo anachopanga sasa anaamini kitatimia kwani amechoka na wezi wa mapenzi ambao mwisho wa siku wanaachana kwa vita na maneno ya kudhalauliana.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts