Home » , » "UBORA WA KAZI ZANGU UNAJULIKANA ,HIVYO SIHITAJI KUJITANGAZA KAMA WAFANYAVYO MASTAA UCHWARO".....ZAMZAM

"UBORA WA KAZI ZANGU UNAJULIKANA ,HIVYO SIHITAJI KUJITANGAZA KAMA WAFANYAVYO MASTAA UCHWARO".....ZAMZAM

Written By JUMA MPEKUZI on Thursday, November 1, 2012 | 7:51:00 AM


MSANII wa filamu za kibongo asiye na matukio ya ajabu Zamzam Salim ‘Zamzam’, amedai kuwa haoni sababu ya kutangaza anataka kulipwa kiasi gani katika kila filamu kwani anaamini ubora wa kiwango chake ndio jibu sahihi kwa waandaaji kwani hataki ufuata mkumbo kama wale ambao kila siku wanajitangaza wakati ukitazama viwango vyao si vya kutisha.

Sasa umeibuka mtindo kwa kila msanii anayejiona staa kutangaza dau analotaka kulipwa katika filamu wakati wengine hajawafikia hatua hata ya kuitwa ‘Professional Actor/Actress’ au kufikia kiwango cha kujulikana hata Afrika Mashariki.


Msanii huyo aliongea na mtandao huu
katika mahojiano mafupi na ndipo aliposema kuwa huwa anakaa na kuwaza ni kitu gani kitakachomfanya alipwe pesa nyingi katika kila filamu anayocheza na jibu ambalo huwa analipata ni kuongeza ubunifu katika kazi anazofanya.

Alisema kuwa wasanii wanaotangaza kutaka kulipwa kiasi fulani cha pesa ni wale ambao wanajiona mastaa kwa sababu ya kutokea kila siku kwenye vyombo vya habari huku wengine wakitokea kwa mambo ya ajabu basi tayari wanajiweka kwenye ubora wa hali ya juu.


Aliongeza kuwa ameshacheza filamu nyingi na zote zimempa umaarufu ikiwemo
Lovers Island’ na nyingine kibao lakini hajafikilia hatua ya kutangaza dau la kulipwa kwani anaamini waandaaji watamtumia kwenye filamu zao kutokana na kiwango chake na si urembo wake au kujulikana kwa sababu ya skendo.

“Mara nyingi huwa napenda kujituma kwa sababu hiyo ndiyo njia ambayo itanifanya mimi niweze kulipwa pesa nyingi katika kila filamu ninazofanya, na sidhani kama nikijulikana sana kwa kupitia skendo ndo naweza kubadilisha maisha yangu na kutaka nilipwe kiasi fulani au kwa sababu ya uzuri, nitalipwa kulingana na kiwango changu kwenye kazi,”
alisema.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts