Home » , , » JB MPINA NDANI YA UZINDUZI WA ALBAMU YA KWANZA YA MASHUJAA BAND

JB MPINA NDANI YA UZINDUZI WA ALBAMU YA KWANZA YA MASHUJAA BAND

Written By JUMA MPEKUZI on Tuesday, November 20, 2012 | 11:20:00 AM


Bendi ya muziki wa Dansi Mashujaa band “watoto wa mama sakina” imekamilisha mipango ya uzinduzi wa albamu yao ya kwanza itakayokwenda kwa jina la Risasi kidole ambapo msanii JB Mpiana wa Wenge BCBG amealikwa kuwa mtumbuizaji mwalikwa katika uzinduzi huo.


Akiongea na vyombo vya habari Rais wa Bendi hiyo Charles Gabriel almaarufu kama Chalz Baba alisema Nguli wa dansi barani Afrika, JB Mpiana, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), anatarajiwa kutua nchini Novemba 26, kwa ajili ya kupamba uzinduzi wa albamu ya Mashujaa Band itakayozinduliwa kwenye viwanja vya Leaders Club, hapa Jijini Novemba 30, mwaka huu.

Kwa sasa mwanamuziki huyo anayetamba na albamu yake mpya iitwayo Biloko, anatarajiwa kuwapagawisha 

Watanzania na rapu yake mpya iitwayo ‘Amataka na Punda’ yaani Panda Punda, ambayo kwa Congo ni gumzo hivi sasa.
Chalz Baba alisema, maandalizi ya onesho lao yanaendelea vizuri kwa ujumla na wanamuziki wako tayari kuwapa raha Watanzania siku hiyo, huku wakitarajia kuingia kambini wiki hii nje kidogo ya jiji.

Alisema albamu yao wanayozindua iitwayo ‘Risasi Kidole’ ina nyimbo sita, ambazo ni ‘Risasi Kidole’ yenyewe ikiwa ni utunzi wake mwenyewe: ‘Ungenieleza’ kazi ya Raja Ladha, ‘Umeninyima’ wa Freddy Masimango, na ‘Hukumu ya Mnafiki’ utunzi wake Jado FFU.

Nyingine ni ‘Kwa Mkweo’ utunzi wake Baba Isaya na ‘Penzi la Mvutano’, ambao umetungwa na Masoud Namba ya Mwisho.
Wanamuziki wengine watakaopamba uzinduzi huo ni pamoja na MB Dogg, H. Baba, Ney wa Mitego na wengineo ambao watajulikana baadaye.

Uzinduzi huo, umeandaliwa na kampuni ya Qs Mhonda, kupitia kwa Mkurugenzi wake Joseph Mhonda, ambaye amesisitiza kuwa kila kitu kiko sawa na kinachosubiriwa ni JB Mpiana kutua kwa ajili ya shoo hiyo tu.

Naye wakala wa JB Mpiana, Guyguy Kiangala, amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo na kuona ubora wa JB Mpiana akichuana na Mashujaa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts