Home » , » NAY WA MITEGO AKANA KUTOKA KIMAPENZI NA NISHA

NAY WA MITEGO AKANA KUTOKA KIMAPENZI NA NISHA

Written By JUMA MPEKUZI on Tuesday, November 13, 2012 | 8:14:00 PM


WAKATI watanzania wengi wakiamini kuwa msanii Ney Wa Mitego, yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanadada wa kwenye tasnia ya filamu Salma Jabu ’Nisha’, mkali huyo amekanusha uwepo wake kwenye mahusiano na mwanamke yeyote na kudai kuwa kwa sasa ana marafiki tu wa kike wa kubadilishana mawazo na si wapenzi au mpenzi kama watu wanavyodai.

Hata hivyo kauli ya msanii huyo inaweza kuzua utata mkubwa kwani mashabiki wake wengi wanajua kuwa mpenzi wake ni mwanadada huyo wa bongo movie ingawa tangu kutoka kwa habari hizo hakuwahi kuzungumza lolote juu ya mahusiano hayo kama ni kweli.


“Hapana kwa sasa sina mpenzi, nimeshatoka na wanawake kadhaa hilo lipo wazi lakini kwa sasa natafuta yule mpenzi mwenye tabia njema,”
alisema.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts