Home » , » "SIJAWAHI GAWA PENZI LANGU KWA SLIM"- BABY MADAHA.

"SIJAWAHI GAWA PENZI LANGU KWA SLIM"- BABY MADAHA.

Written By JUMA MPEKUZI on Wednesday, January 16, 2013 | 5:56:00 AM

MWANADADA mwigizaji wa filamu na mwanamuziki Baby Madaha amekanusha kuwa na uhusiano na mwigizaji mwenzake wa filamu Slim baada ya habari za uhusiano wao kuvuma na kusababisha ugomvi na mzazi mwenzake Slim ambaye pia ni rafiki yake Baby Madaha, msanii huyo amedai kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na Slim bali alimshirikisha katika video ya wimbo wake tu.

baby Madaha
Baby Madaha
“Maneno mengi yanasemwa lakini ukweli ni kwamba sina uhusiano na Slim bali kilichotokea nilikuwa natengeneza video yangu ya muziki na nilihitaji kumpata mwanaume mwenye muonekano mzuri na mrefu kama Slim kwa hiyo kishemeji shemeji nikafanya naye kazi kama msanii mwenzangu na shemeji yangu,”anasema Baby Madaha.

Lakini jambo la ajabu rafiki yake ambaye ndio mzazi mwenzake na Slim alikasirika na kutengeneza bifu akijua anatoka naye, Baby Madaha akisema lakini pia baadae aligundua kuwa tayari rafiki yake huyo alikuwa ametengana na Slim, Madaha anasema kuwa yeye hana mwanaume yoyote na hataki mwanaume zaidi ya maisha yake ya Single

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts