Home » » HUYU NDO ASKARI ALIYEPEWA "KIPIGO KIKALI" WAKATI WA MAANDAMANO YA WANAFUZI WA IFM

HUYU NDO ASKARI ALIYEPEWA "KIPIGO KIKALI" WAKATI WA MAANDAMANO YA WANAFUZI WA IFM

Written By JUMA MPEKUZI on Tuesday, January 15, 2013 | 2:27:00 PMJeshi la Polisi linaonekana kufanya kazi zaidi kwa mazoea kuliko kuzingatia mafunzo wanayopewa, pichani ni askari polisi aliyejeruhiwa na wenzake baada ya kupigwa marungu kwa kutomjua kama nayeye ni askari hadi alipopiga kelele ‘mtaniua mimi mwenzenu’ ndipo wakamuachia. 

 Kilichofuata baada ya askari huyo kuachiliwa na wenzake alimalizia hasira zake zote kwa wanafunzi hao kwa kutembeza kipigo (mkong’oto) mkali kwa wanafunzi Chuo Cha IFM waliojaribu kutaka kulazimisha jeshi la polisi kufanya mkutano mbele ya kituo cha Polisi Kigamboni badala ya kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava Kigamboni bila kujali kuwa wanafunzi hao walikuwa wakikabiliana na moshi nzito wa mabomu ya machozi lakini pia walisha kuwa chini ya ulinzi mkali na hakukuwa na sababu yeyote ya kuwapiga hivyo. 

Mbali na askari huyo kulikuwepo na askari wengine wawili akiwemo mmoja wakike nao pia waliambulia kipigo hicho.  
---------------------------------------------------------------------
Fuatilia picha za Askari huyo na matukio aliyofanya .

Picha hii inakuonesha kwa karibu namna rungu lilivyompasua Askari huyu, hapa utapata picha kama huyu askari aliyepigwa kidogo tu baadaye akaachiwa ameumia hivi je wale waliopata mkong'oto wapo kwenye hali gani.

Hapa anazuia damu sehemu aliyopigwa isindelee kuvuja kwa kutumia kitambaa.

Baada ya kupata nafuu anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa kumkamata mmoja na kumpa kipigo cha nguvu hadi askari wenzake walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi huyo.

Hakuishia hapo aliwafuata pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na kumpa kipigo vile alivyojiskia ili amalizie hasira zake.

Kumbuka kipigo hicho kinafanyika mbele ya kituo cha polisi huku kukiwa na ulinzi mkali umeimarishwa.

Alichagua kama maembe au mpira na kuchezea alivyotaka!

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts