Get the latest updates from us for free

Home » , » LULU MICHAEL AKATAA KUFANYIWA "SHEREHE" YA KUPONGEZWA KUINGIA URAIANI

LULU MICHAEL AKATAA KUFANYIWA "SHEREHE" YA KUPONGEZWA KUINGIA URAIANI

Written By JUMA MPEKUZI on Wednesday, January 30, 2013 | 7:28:00 PMJanuary 29 2013 ndio msajili alithibitisha kwamba mwigizaji Lulu ametimiza masharti yote ya dhamana juu ya kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia na hivyo  kumwachia  kwa dhamana.....
 
Lulu na mama yake mzazi wote kwa pamoja waliangua vilio baada ya dhamana yao kukamilika wakati wakiwa nje ya Mahakama kabla ya kuondoka na Lulu kuingia uraiani.

Kabla  ya dhamana  hiyo kulikwa  na  tetesi  kwamba  Lulu angefanyiwa  sherehe kubwa  ya  kupongezwa  kuja uraiani.

Kwa mujibu wa ndugu yake  wa karibu, Lulu amegoma  kufanyiwa sherehe  na  badala  yake jana aliwaomba  watanzania  wamuombee  kwa  mungu  maana  kesi bado inaendelea.....
 
 “Nawashukuru watu wote na nilikua naomba watu waendelee kuniombea sababu hii ni dhamana tu lakini kesi bado ina safari ndefu… nawashukuru wale wote waliokua na mimi kwa hali yeyote ile na zaidi zaidi namshukuru sana Mwenyezi Mungu”....LULU
Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts