Home » , , » PICHA ZINAZOONYESHA TATTOO MPYA YA MSANII RAYUU PAMOJA NA NGUO ZA NDANI ZASAMBAA TENA

PICHA ZINAZOONYESHA TATTOO MPYA YA MSANII RAYUU PAMOJA NA NGUO ZA NDANI ZASAMBAA TENA

Written By JUMA MPEKUZI on Tuesday, January 15, 2013 | 8:52:00 PM

WAKATI wadau wa tasnia ya filamu wakitarajia kuona tasnia hiyo ikiwa imebadilika hali bado tete, ambapo msanii ‘Rayuu’, ameanza vituko kwa kuonesha tattoo yake mpya huku akiwa kwenye pozi tata ambalo linamuonesha hadi nguo yake ya ndani.

Msanii huyo mwaka uliopita aliandamwa na skendo ya kutembea na mwanaume wa mtu pamoja na ishu kadhaa, lakini mbali na haya bado mwaka huu anaonekana kuwa moto wa kuotea mbali.


Mwandishi wetu alifanya mchakato wa kumtafuta ili kuzungumza naye juu ya ujio huo ambao unaweza kuleta maneno mtaani, ambapo alidai kuwa hakuna mtu anayeweza kumzuia katika jambo analotaka kulifanya.


Alisema kuwa picha hiyo haimanishi kwamba anavunja maadili ingawa baadhi ya watu wanaamini hivyo, pale wanapoona tattoo ama nguo ya ndani.


“Ni kweli nimepiga picha ambayo inanionesha sehemu kubwa ya kiuno changu pamoja na nguo yangu ya ndani lakini halimanishi kwamba mimi ni muhuni au navuja maandili hapana ni kitu kidogo sasa ningevua nguo kabisa ingekuaje,” alidai msanii huyo bila haya.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts