Get the latest updates from us for free

Home » , , » ROMA MKATOLIKI AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA KUNDI LA KINA JOH MAKINI.

ROMA MKATOLIKI AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA KUNDI LA KINA JOH MAKINI.

Written By JUMA MPEKUZI on Monday, January 7, 2013 | 8:01:00 AM

Rapper Roma Mkatoliki ambae ni mzaliwa wa 96.0 Tanga ameitii kiu ya mashabiki wengi wa hip hop waliotaka kujua siku akifungua kinywa chake kuhusu kundi la WEUSI atasema nini.

Wakati akiizungumzia single yake mpya ya 2030 Roma alitumia hiyo nafasi pia kuweka wazi kwamba haba beef wala chuki na kundi la Weusi na kama vile haitoshi akatolea mfano status aliyoiandika kwenye page yake ya facebook siku kadhaa kabla ya kuwasifia WEUSI kwa show yao ya mwaka pale Maisha Club.
Joh Makini na Nikki wa II siku ya show december 23 2012.
Japo anasema baada ya kuiandika hiyo status kuna ambao walimuunga mkono na waliompinga, namkariri akisema

 “kuna waelewa na wasio waelewa… mara nyingi tumfatilishe yule muelewa, kitu kikiwa kizuri mimi ni mtu wa kukubali, ndio hivyo nilivyoumbwa haiwi kwa njia ya unafiki au kwa kutafuta kitu kingine chochote, ile show ya WEUSI ilikua kali mi Maisha Club nakwenda sana kwenye show nyingi lakini ilikua ni show nzuri jinsi ilivyopangiliwa, haikupata watu wengi sana kama nilivyotarajia lakini hata waliofika inatosha, kikubwa nilichokipenda ni show ambayo haikumuhusisha msanii mwingine yeyote… walifanya show nzuri kuanzia Lord Eyez, Nikki, Bonta, G alitisha sana Joe mwenyewe alifanya vizuri, haikuniboa hata kidogo”

“Jana yake usiku kabla ya show nilikua nao kina Lord na G nikapiga nao stori lakini once wanapofanya mistake kwenye game unagundua hapa wamekosea hilo pia sitalifumbia macho nitaweza kuliongea, kama unakuta 50 na Jay Z wanabeef lakini tunashangaa 50 anapoperform Jay Z anaamka kwenye kiti kabisa anapiga makofi anaonekana ana mzuka, mawazo ya watu tu kwamba labda watu wakiwa na utofauti basi siwezi kukubali mtu akifanya vizuri, mbali na hivyo vyote nilivyoviongea hakuna matatizo kati ya Roma na wale watu, najiona niko sawa sina matatizo na mtu yeyote mbali hata na wale pale” – Roma Mkatoliki

Hii ndio status ya Roma Mkatoliki dec 13 2012.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts