Get the latest updates from us for free

Home » , , , » "SIHITAHI SAMAHANI YAKO...SIJUI NIKU- DELETE?"...HUU NI UJUMBE MZITO WA WEMA SEPETU KWA AUNT EZEKIEL

"SIHITAHI SAMAHANI YAKO...SIJUI NIKU- DELETE?"...HUU NI UJUMBE MZITO WA WEMA SEPETU KWA AUNT EZEKIEL

Written By JUMA MPEKUZI on Thursday, January 17, 2013 | 8:18:00 PM


WACHEZA sinema wenye majina makubwa Bongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ wameingia kwenye bifu zito na kuwafanya wasisalimiane.....


Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, bifu la wawili hao lilianza usiku wa kuamkia Januari Mosi, mwaka huu baada ya Wema kumwalika Aunt kwenye sherehe ya kuukaribisha mwaka lakini pamoja na kuupokea mwaliko huo, Aunt hakutokea nyumbani kwa Wema ilikofanyika shughuli hiyo iliyopambwa na vyakula na vinywaji.


Awali, Wema alipoona Aunt anachelewa kufika kwenye shughuli hiyo, aliamua kumpigia simu mara kwa mara na kupewa matumaini ya kuvuta subira.


Ilipotimu saa 6:01 usiku bila ya Aunt kuonekana, Wema alimtumia ujumbe mzito kupitia mtandao wa BBM na Aunt akaanza kuomba radhi.


Ujumbe wa Wema ulisomeka hivi: “Hata sina hamu na wewe ila Happy New Year, sihitaji samahani yako sijui niku-delete?” akimaanisha amuondoe kwenye orodha ya marafiki zake wa karibu. 


Mbali na ujumbe huo, Risasi lina meseji za Aunt akimuomba radhi Wema kutokana na kutofika kwenye sherehe hiyo.


Inadaiwa kuwa Wema alikasirika na kuhisi kwamba Aunt aliungana na baadhi ya wasanii wengine wa Bongo Movie ambao hakuwaalika kwenye shughuli yake kutokana na kupishana nao Kiswahili siku za nyuma.


Asubuhi yake, Aunt aliandika kwenye mtandao wa BBM: “ Chondechonde my luv, nimekosea mamy naomba unisamehe, naomba msamaha mbele ya hadhara.” 


Pamoja na kuombwa radhi, Wema hakujibu kitu zaidi ya kumpotezea rafiki yake huyo aliyemsaidia kufanikisha sherehe ya harusi yake iliyofanyika miezi michache iliyopita.


Juzikati, mastaa hao walikutana kwenye arobaini ya mama wa Mtangazaji wa Redio na Runinga za Clouds, Zamaradi Mketema na wakashindwa hata kupeana salamu, kila mmoja alimchunia mwenzake.


Mama mzazi wa Wema aliendelea kumpiga stop mwanaye kwa kuwakumbatia marafiki, akamwambia kuwa hana marafiki wa kweli.


Wema alipotafutwa , alishindwa kuweka wazi moja kwa moja kuwa haelewani na Aunt na kudai kuwa hana muda wa kuongelea mambo hayo.


Kwa upande wake, Aunt alikataa kutoa ushirikiano na kukata simu mara baada ya kuulizwa swali kuhusiana na urafiki wake na Wema.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts