Home » , » "KAZI ZANGU HUNIFANYA NIKOSE HAMU YA PENZI"...NISHA

"KAZI ZANGU HUNIFANYA NIKOSE HAMU YA PENZI"...NISHA

Written By JUMA MPEKUZI on Wednesday, January 9, 2013 | 8:36:00 PM


WAKATI ndoa nyingi zikivunjika kwa sababu ya mmoja kuwa bize na kazi na kushindwa kumjali mwenzake, msanii anayetesa na filamu yake ya ‘Pusi na Paku’ Salma Jabu ’Nisha’, amesema kuwa amekuwa akifanya kazi sana huku akisahau kama kuna mapenzi na hiyo inatokana na majukumu mazito aliyonayo katika kazi zake.

Mwandishi wetu baada ya msanii huyo kudai hivyo alimuuliza swali kuwa endapo angekuwa yupo kwenye ndoa si angekuwa anaachika mara kwa mara, alidai kama angekuwa kwenye ndoa angejirekebisha na angepanga muda wake vizuri kwani mume naye ana nafasi yake.


Alisema kuwa siku za karibuni amekuwa bize kutokana na maandalizi ya kuitoa filamu yake hiyo mpya, ambayo tayari ipo sokoni huku ikiwa inafanya vizuri. Aliongeza kuwa mara kadhaa amekuwa akisemwa na mpenzi wake lakini hiyo hampi shida kwani anachikifanya ni kutafuta pesa.


“Naweza kusema mwishoni mwaka mwaka jana nilikuwa bize kiasi kwamba hata kurudi nyumbani nilikuwa narudi usiku sana, kazi zilikuwa nyingi kiasi  cha kushindwa hata  kumhudumia mpenzi wangu  lakini nashukuru Mungu kwamba mambo yanaenda sawia” alisema.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts