Get the latest updates from us for free

Home » , » MR. BLUE ATUPIWA VITU VYAKE NJE NA NHC BAADA YA KUFANYA "UFISADI" WA CHUMBA

MR. BLUE ATUPIWA VITU VYAKE NJE NA NHC BAADA YA KUFANYA "UFISADI" WA CHUMBA

Written By JUMA MPEKUZI on Saturday, February 2, 2013 | 1:26:00 PM


Familia ya staa wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr. Blue’, imeingia kwenye kashikashi baada ya kuvunjiwa nyumba na kutupiwa vitu nje, Risasi Jumamosi linashuka nayo.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘mwandishi’ wetu lilijiri Januari 30, mwaka huu, Posta, jijini Dar katika Ghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambayo Mr. Blue alikuwa amepanga na ndugu zake akiwemo mjomba wake (jina halikupatikana).


Kwa mujibu wa chanzo makini, Mr. Blue na mjomba wake walipangisha chumba kimoja kwenye ghorofa hiyo kwa miaka mingi iliyopita kisha wakaamua kuiba chumba kingine ambacho kilikuwa hakina mpangaji.

“Walitoboa mlango kwenye chumba ambacho kilikuwa hakitumiki, wakaanza kukitumia bila kukilipia hivyo jamaa wa NHC walipotimba wakatoa vyombo vyote nje,” kilisema chanzo.


Ilifahamika kuwa siku ya tukio wamiliki (NHC) walivamia na kuvunja mlango kwa kuwa Mr. Blue hakuwepo na aliporudi alikuta zoezi la kutoa vyombo likiendelea.


Alipoulizwa na Mwandishi wetu aliyefika eneo la tukio, kuhusiana na sakata hilo, Mr. Blue alikiri kutolewa vyombo nje na kudai hakuna tatizo kwani alivipelekwa kwa mjomba wake.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts