Home » , » Lady Jay Dee Azungumzia Msanii wa Kiume Anayemfikiria Kushirikiana Nae

Lady Jay Dee Azungumzia Msanii wa Kiume Anayemfikiria Kushirikiana Nae

Written By Bigie on Saturday, April 2, 2016 | 5:27:00 PM

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lady Jay Dee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Ndi ndi ndi’ amefunguka na kuweka wazi wazi msanii wa kiume ambaye kwa sasa anamfikiria katika kufanya nae kazi.
 
Kupitia Account yake ya twitter ambapo alitoa nafasi ya maswali kutoka kwa mashabiki zake Lady Jay Dee aliulizwa swali kama ataweza kufanya remix ya wimbo wake mpya na kama atafanya hivyo anadhani ni msanii gani wa kiume ambaye ataweza kufanya nae kazi hiyo. Ndipo hapo aliposema kwa sasa anamfikiri sana Mr Blue.
“Kiukweli mtu niliemfikiria hapo ni Mr Blue, naona ndio ata fit vizuri zaidi, Msanii wa Tanzania alieko akilini kwangu hivi sasa ni Mr Blue” alisisitiza Lady Jaydee
Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi sababu za ukimya wake kwenye muziki kabla ya kuja na wimbo huo mpya na kusema kuwa huo ndio utaratibu wake toka amenza muziki na toka anatoka na Album ya kwanza mwaka 2001 yeye si mtu ambaye anatoa ngoma mara kwa mara bali huwa anajipa muda wa kujiandaa lakini hata hivyo nyimbo anazokuwa anatoa zinadumu muda mrefu ndiyo maana anakosa sababu ya kuharakisha kutoa kazi kila siku.
 
“Ndio utaratibu niliojiwekea miaka yote tangu Album ya kwanza 2001, mimi huwa sio msanii wa back to back lakini uzuri nyimbo zenyewe hudumu miaka mingi hivyo nakosa sababu ya kuharakisha kutoa kazi kila siku. Zitakapoisha nyimbo zilizomo kwenye album hii ya 7 itachukua muda tena kutoa zingine. Huwa najiandaa” alisema Lady Jay Dee

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts