Home » , , » Ukaribu wa Agness Masogange na Kidoa wazua sintofahamu

Ukaribu wa Agness Masogange na Kidoa wazua sintofahamu

Written By Bigie on Saturday, April 2, 2016 | 5:46:00 PM


Video Queen nyota, Agnes Gerald maarufu kama Masogange anadaiwa kutaka kumharibu muuza nyago chipukizi Asha Salum ‘Kidoa’ baada ya wadau kutilia shaka ukaribu wao.
 
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, katika siku za hivi karibuni mabinti hao wamekuwa na urafiki wa karibu, wakichati mambo mengi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, kitu kinachoonesha huenda ushosti wao ukafika mbali zaidi ya hapo.
 
“Si unajua Masogange ana zile dili zake za kwenda mara kwa mara Sauz huku ikiwa haijulikani hasa anafuata nini? Na si unakumbuka ule msala wake wa kukamatwa na madawa ya kulevya? Sasa wadau wanahofu asije naye akaingizwa kwenye mchongo,” kilisema chanzo hicho.
Kidoa katika pozi
Katika kuweka sawa madai hayo, tulimtafuta Kidoa ambaye alifunguka; “Mimi ni mtu mzima na akili zangu timamu, siyo kila rafiki utakayekuwa naye basi lazima uige tabia zake, halafu Masogange siyo rafiki yangu kihivyo, kawaida tu!”
 
Kwa upande wake, Masogange alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo, alijibu kwa kifupi; “Ulishawahi kuniona nikienda naye Sauz, au ulishawahi kuniona naye kwenye ndege, kifupi mimi sinaga rafiki.”


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts