Home » » Atiwa Mbaroni Kwa Kumbaka Mtoto wa Miaka Saba.

Atiwa Mbaroni Kwa Kumbaka Mtoto wa Miaka Saba.

Written By Vuvuzela on Friday, May 20, 2016 | 12:48:00 PM

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mkazi wa eneo la Bombambili, Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kukutwa akimbaka mtoto wa miaka saba anayesoma darasa la pili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei 18 mwaka huu saa 11 jioni nyumbani kwao na mtoto huyo.

Alifafanua kuwa siku ya tukio mkazi huyo alikwenda sehemu hiyo kuangalia runinga sebuleni na baada ya muda mfupi binti huyo alirejea nyumbani akitokea shule.

“Msichana huyo alikuja sebuleni kuangalia runinga wakati huo wafanyakazi wa ndani wa nyumba hiyo walikuwa nje na ndipo kijana alipopata mwanya wa kufanya ukatili huo,” alisema kamanda.

Alisema baada ya muda mfupi kupita, mfanyakazi wa kike aliingia sebuleni ghafla na kumkuta akimbaka mtoto huyo.

Alifunga mlango, kisha aliwaita majirani na viongozi wa Serikali wa mtaa huo.

Kamanda alisema wananchi walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka polisi. Pia, mtoto huyo alichunguzwa na madaktari walithibitisha kuwa aliingiliwa kimwili na kuharibiwa sehemu zake za siri.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts