Home » » Zaidi Ya Tani 500 Za Sukari Zatolewa jijini Mwanza.

Zaidi Ya Tani 500 Za Sukari Zatolewa jijini Mwanza.

Written By Vuvuzela on Wednesday, May 25, 2016 | 11:34:00 AM

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wake umepokea Tani 500 za Sukari, zikitokea kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji na Msambazaji P.H Shah.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei elekezi , na kusema kuwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa nipamoja nakufikishwa katika vyombo vya dola.

Mongella amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la sukari na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie maelekezo bila kuvunja utaratibu utakao wekwa.

Mahitaji ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 ukweli kwamba itasaidia kupunguza uhaba wa sukari unao ukabili mkoa huu kwa sasa.

Hata hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema, tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na kwamba muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts