Get the latest updates from us for free

Home » » CCM Yaishukia CHADEMA

CCM Yaishukia CHADEMA

Written By Vuvuzela on Tuesday, June 7, 2016 | 8:11:00 AM


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekishukia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa hatua zao za kutaka kwenda kuishitaki serikali kwa wananchi juu ya hatua, ambazo zimekuwa ikichukua za kuziba mianya ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.

Kimesema ni lazima watu wahoji kama Rais John Magufuli, anafanya mambo yenye maslahi mapana kwa taifa lakini Chadema inadai ni udikteta, kinafanya hivyo kwa maslahi ya nani, kimetumwa na nani na kinafadhiliwa na nani.

Hayo yalielezwa jana na Msemaji wa Chama hicho, Christopher ole Sendeka wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Chama hicho zilizopo Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.

Alisema ni jambo la ajabu kuona wakati serikali inashughulika na walanguzi wachache, ambao wamekuwa wakilikosesha taifa mapato, kikundi cha watu wachache wanaenda kukisemea kikundi hicho na kuitaja Tanzania kama nchi ya kifashisti na kidikteta jambo ambalo si sawa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts