Get the latest updates from us for free

Home » » Kijana Aliyelelewa na Nyati Mbaroni kwa Tuhuma za Kubaka na Kulawiti

Kijana Aliyelelewa na Nyati Mbaroni kwa Tuhuma za Kubaka na Kulawiti

Written By Vuvuzela on Saturday, June 11, 2016 | 6:31:00 PM


KIJANA aliyelelewa na nyani kwa takribani miaka nane baada ya kuzaliwa na kutupwa porini mkoani Shinyanga na kuokolewa katikati ya miaka ya 2000, Baraka Joshua amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Ilala, akikabiliwa na mashitaka ya kulawiti na kubaka.

Joshua maarufu kama mtoto wa nyani, alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja. Akisomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali Florida Wenceslaus, alidai Mei 17, mwaka huu eneo la Shule ya Msingi Tabata Kimanga, wilayani Ilala mshtakiwa alimlawiti mtoto mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa).

Wenceslaus alidai katika mashitaka ya pili, siku hiyo mshitakiwa alimbaka mtoto huyo ambaye alikuwa anasoma katika shule ya msingi Kimanga. Mshtakiwa alikana mashitaka yote na kwamba amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hakimu Kioja aliyataja masharti ya kuwa awe na wadhamini wawili kati yao mmoja awe mtumishi wa Serikali watakaotia saini ya Sh milioni mbili kila mdhamini, kesi itatajwa Mei 26, mwaka huu. Inaelezwa kuwa awali mshtakiwa alikuwa anaishi na nyani kabla hajachukuliwa na watu wa Maliasili baada ya kumfuatilia kwa karibu.

Ilidaiwa mshitakiwa alipochukuliwa na watu hao alifikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kuanza kutibiwa kwa kufundishwa namna ya kutembea. Mshtakiwa alikuwa amezoea maisha ya nyani, kwani alikuwa anatembea kama nyani na kuongea sauti ya nyani.

Baada ya kutibiwa alitokea msamaria mmoja ambaye alikuwa anaishi naye na aliamua kumpa Joshua biashara ndogo ya kufanya katika shule ya msingi Kimanga ambapo inadaiwa ndiko alikombaka mtoto huyo.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts