Get the latest updates from us for free

Home » » Makamu Wa Rais Mhe. Samia Akutana Na Rais Wa Comoro Pamoja Na Balozi Wa Japan Nchini Jijini Dar Es Salaam

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Akutana Na Rais Wa Comoro Pamoja Na Balozi Wa Japan Nchini Jijini Dar Es Salaam

Written By Vuvuzela on Tuesday, June 28, 2016 | 8:58:00 PM


Rais wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusianona ushirikiano wa kihistoria  kati ya Tanzania  na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na biashara.

Rais huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya  kuendelea na safari yake ya Mecca – Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.
Rais  Azali Assouman pia amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tanozinazolenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii nakusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Komoro.

Akitoa ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI kwa Rais wa  Comoro Azali assouman, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Rais wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo MBILI hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo MBILI.
  
 
Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa Comoro kheri katika safari yake ya Mecca– Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.
 
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa nchini Masaharu Yoshida na kumweleza kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha mazingira bora kwa ajili ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo wawekezaji kutoka
nchini  JAPAN.
 
Makamu wa Rais amesema serikali ya JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania Bara na Visiwa hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji na kusema jambo hilo ni zuri na lakuigwa na washirika wengine wa maendeleo.
 
Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHINDA amemhakikishia Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea kufadhili  ipasavyo miradi ya maendeleo hapa nchini ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts