Get the latest updates from us for free

Home » » Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Yakusanya Matrilioni ya Fedha Mwezi May

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Yakusanya Matrilioni ya Fedha Mwezi May

Written By Vuvuzela on Tuesday, June 7, 2016 | 7:44:00 AM

 
Ikiwa imewekewa lengo la kukusanya Sh12.054 kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Mei 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kufikia malengo kwa kukusanya Sh1.032 trilioni kwa kipindi cha mwezi uliopita, ikiwa ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo lililowekwa.

Makusanyo hayo yanaifanya Serikali ya Awamu ya Tano iliyoingia madarakani Novemba 5, 2015 kukusanya zaidi ya Sh6.567 trilioni katika kipindi cha miezi mitano. Takwimu zinaonyesha kwamba kuanzia mwezi Desemba, TRA haijakusanya mapato chini ya Sh1 trilioni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, jana, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alisema lengo lao kwa mwezi uliopita lilikuwa ni kukusanya Sh1.025 trilioni na kwamba, kuanzia Julai 2015 hadi Mei 2016 wamekusanya Sh11.956 trilioni.

“TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa fedha na kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo, hususan katika mipaka,” alisema Kidata.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts