Get the latest updates from us for free

Home » » Maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yafutwa

Maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yafutwa

Written By Vuvuzela on Saturday, June 11, 2016 | 6:23:00 PM


Serikali ya Tanzania imebadilisha mfumo wa maadhimisho ya siku ya utumishi wa umma badala yake siku hiyo ya tarehe 16 hadi 23 mwezi huu itatumika kwa watendaji wakuu wa wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na taasisi za serikali kusikiliza kero za watumishi wa umma katika maeneo yao ya kazi kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh. Angellah Kairuki amesema hakutakuwa na maonesho katika viwanja vya Mnazi Mmoja kama ilivyozoeleka kwani bado kuna changamoto nyingi zinazowakabili wafanyakazi na hivyo vyema siku hiyo wakasilizwa ili kutatuliwa.

Aidha katika hatua nyingine waziri Kairuki amesema kuanzia tarehe 1 Machi mwaka huu hadi tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu jumla ya watumishi 12,246 wameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya miashahara kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kutimiza umri wa kustaafu kwa lazima, kufariki au kufukuzwa kazi.

Amesema katika zoezi hilo pia jumla ya shilingi 25,091,292,688,82 zingepotea kama watumishi wasingeondolewa kwenye mfumo ikilinganishwa watumishi 10,295 walioondolewa kwenye mfumo hadi tarehe 30 Aprili mwaka huu na jumla ya shilingi 23,206,547,598.82 zilizookolewa ambapo hilo ni ongezeko la watumishi 1,951 na shilingi 1,884,745,090.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts