Get the latest updates from us for free

Home » » Rais Magufuli Amteua Prof.Bukurura kuwa Mwenyekiti wa TPDC

Rais Magufuli Amteua Prof.Bukurura kuwa Mwenyekiti wa TPDC

Written By Vuvuzela on Saturday, June 4, 2016 | 7:12:00 AM


RAIS John Magufuli amemteua Profesa Sufian Bukurura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia Mei 30, mwaka huu.

Profesa Bukurura anachukua nafasi ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Michael Mwanda.Taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa kwa vyombo vya habari jana ilisema kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewateua wajumbe sita wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC kuanzia Juni 3, mwaka huu hadi Juni 2, 2019.

Aliwataja wajumbe hao kuwa Jaji Josephat Mackanja, Balozi Ben Moses, Profesa Abiud Kaswamila, Profesa Hussein Sosovele, Dk Shufaa Al-Beity na Mwanamani Kidaya.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts