Get the latest updates from us for free

Home » » Sugu ndani ya Tuhuma ya Kuwanyooshea Kidole Wabunge wa CCM

Sugu ndani ya Tuhuma ya Kuwanyooshea Kidole Wabunge wa CCM

Written By Bigie on Friday, June 10, 2016 | 7:18:00 PM


 Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameitaka Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma dhidi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu anayedaiwa kuwaonyeshea kidole cha kati wabunge wa CCM.

Sugu anadaiwa kufanya kitendo hicho June 6, mwaka huu alipokuwa akitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuhusu azimio la bunge kuridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.

Naibu Spika ameitaka kamati hiyo kumchukulia hatua kali kama watamkuta na hatia ya kufanya kitendo hicho

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts