Get the latest updates from us for free

Home » » Wabunge na wananchi wazungumzia bajeti kuu ya serikali inayotarajiwa kusomwa Leo

Wabunge na wananchi wazungumzia bajeti kuu ya serikali inayotarajiwa kusomwa Leo

Written By Vuvuzela on Wednesday, June 8, 2016 | 9:08:00 AM

 
Baadhi ya wabunge na wananchi wameelezea mategemeo na mitizamo yao katika bajeti ya serikali inayotarajiwa kusomwa leo bungeni ambapo wengi wao wamesema bajeti hiyo itawasaidia kama itapungunza gharama za maisha sambamba na kuwasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma bora za maendeleo.


Dotto Biteko ni mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye anasema ni wazi kuwa bajeti ya sasa itawaweza kuleta mabadiliko ya moja kwa moja kwa watu wake kwa sababu sehemu kubwa ya fedha zimetengwa kwa ajili ya  miradi ya maendeleo.
 
Maelezo hayo yanatofautiana na yale ya Mh Abdadalh Mtolea mbunge wa Temeke kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF ambapo anasema bajeti hi haiwezi kuwafikisha wananchi sehemu yoyote kwani  inasisitiza uchumi wa viwanda lakini hakuna hata shilingi moja iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.
 
Mh Stepheni Ngonyani ni mbunge wa Korogwe vijijini ambaye anasema wananchi wanachotaka ni kuona bajeti itakayowasilisihwa inajibu kero mbalimbali kama kupungua kwa bei za bidhaa mbalimbali kama Sukari, Misamaha ya kodi sambamba na uboreshwaji wa huduma za kijamii.
 
Naye waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za serikali za mitaa Mh George Simbachawene amesema bajeti inayotarajiwa kusomwa bungeni wananchi wanapaswa kujua kuwa serikali inategemea kodi katika kuitekeleza na hivyo wahakikishe wanalipa kodi kwa wingi ili bajeti ziweze kutekelezeka kiurahisi.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts