Get the latest updates from us for free

Home » » Wataka uchunguzi ugonjwa ulioua watu 7 Dom

Wataka uchunguzi ugonjwa ulioua watu 7 Dom

Written By Vuvuzela on Thursday, June 23, 2016 | 5:08:00 PM


WAKAZI wa Kijiji cha Mwaikisabe Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kufanya uchunguzi juu ya ugonjwa ulioibuka na kuua watu saba, wakiwemo watatu wa familia moja huku zaidi ya wagonjwa 20 wakiwa wamelazwa hospitali.

Walisema watu wengi bado wanahisi kuwa ugonjwa huo umesababishwa na nyama ya ng’ombe.Wakizungumza mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliyekuwa ameongozana na timu ya wataalamu, mkazi wa Mwaikisabe, Abbas Mussa alisema serikali iwe wazi juu ya ugonjwa huo uliosababisha vifo kwenye familia moja, licha ya kuwa nyama hiyo inadaiwa kuliwa na wakazi wengi kijijini hapo, lakini waliodhurika ni familia moja tu ambayo ilipoteza watoto watatu kwa wakati moja.

Abbas aliyesema ni miongoni mwa waliokula nyama hiyo, haoni sababu serikali kushindwa kutoa majibu ya ugonjwa huo unaoitwa wa ajabu wakati wakazi wengi wamekula nyama hiyo, lakini hawajaathirika. Mkazi mwingine, Mwajuma Selemani alishangaa kwa nini serikali imekuwa wazito wa kutoa majibu wakati imebainika wazi nyama hiyo kusababisha vifo vya watu hao.

“Cha kusikitisha hata wanyama kama mbwa, paka wamekufa baada ya kula nyama hiyo,” alisema.

Akizungumza na wananchi hao, Waziri Ummy aliwatoa hofu wananchi walioathirika na ugonjwa ambao haujajulikana na sasa serikali imepeleka wataalamu mbalimbali wa afya ambao wamekwishachukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi na hivi karibuni watatoa majibu baada ya uchunguzi kukamilika.

Mbali na kuzungumza na wananchi hao, pia alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Chemba ambapo wagonjwa 11 wamelazwa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts