Home » » Bosi wa zamani wa Diamond na Rich Mavoko atumbuliwa Kaburu Records

Bosi wa zamani wa Diamond na Rich Mavoko atumbuliwa Kaburu Records

Written By Vuvuzela on Wednesday, July 27, 2016 | 7:49:00 PM

 Kaburu (wa kwanza kulia) akiutambulisha uongozi wake mpya wa Kaburu Record

Uongozi wa ‘Kaburu Records’ studio ya kisasa iliyozinduliwa miezi mitatu iliyopita na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, imemtimua aliyekuwa meneja wa studio hiyo Msafiri Peter ‘Papa Misifa’ kwa madai ya kushindwa kufikia malengo ya kampuni hiyo. 

Akiongea Jumanne hii, Mmiliki wa studio hiyo, Kaburu, amesema wameamua kuachana na bosi huyo wa zamani wa Diamond na Rich Mavoko kutokana na kushindwa kuifikisha kampuni hiyo sehemu ambayo waliafikiana.

“Kaburu Record kama kampuni tumeamua kumsimamisha kazi Msafiri Peter ‘Papa Misifa’ kutokana na kushindwa kuifikisha kampuni yetu sehemu ambayo tulipanga,” alisema Kaburu. “Miezi mitatu sio mingi toka tumtangaze lakini kama kampuni kuna vitu ambavyo tulivipanga kuvifanya ndani ya muda huo lakini mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya utekelezaji, hii ni biashara tumewekeza pesa ili izalishe taratibu lakini tumeona imeshindikana,”

Aliongeza, “Kwa hiyo mimi kama mtu kwenye hisa kubwa kwenye kampuni hii nimeamua kumfuta kazi na kuweka uongozi mpya, Papa Misifa hayupo tena kwenye kampuni hii, ukitaka kufanya kazi na sisi njoo ofisini,”

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts