Home » » CCM Yatoa Kauli Nzito baada ya CHADEMA kutaja siku ya maandamano

CCM Yatoa Kauli Nzito baada ya CHADEMA kutaja siku ya maandamano

Written By Vuvuzela on Thursday, July 28, 2016 | 7:05:00 PM


July 28 2016 Chama cha mapinduzi (CCM) kikiongozwa na msemaji wake Christopher Ole Sendeka  kimekutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kuzungumzia hatua iliyotangazwa na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kufanya maandamano ya nchi nzima.

"Jana tarehe 27/7/2016 chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), walitoa kauli iliyojaa uongo mwingi za kibabaishaji na kuthibitisha ukweli kuwa kwa hakika kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli wapinzani wamekosa ajenda.

"Katika uongo na uzushi walioutangaza, CHADEMA wanasema wameamua kufanya mikutano na maandamano nchi nzima, kimsingi hoja walizozitumia zimejaa upotoshaji na uongo uliokithiri. Ifahamike kuwa serikali haijazuia mikutano kwenye majimbo yao.
 
"Wabunge wako huru kufanya shughuli zao na tumeona baadhi ya wabunge wakifanya shughuli zao majimboni bila shida wakiwemo hao wa upinzani.
 
"Ni vizuri tukakumbuka matukio kwenye operesheni kama hizi yaliyopoteza maisha ya vijana wetu na matokeo ya kila operation" –Ole Sendeka
 

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts