Home » » Event ya ‘Zari All White Party’ yazuiliwa

Event ya ‘Zari All White Party’ yazuiliwa

Written By Bigie on Thursday, July 7, 2016 | 10:43:00 AMZari Hassan maarufu kama Zari the Bossylady kutoka Uganda, na mzazi mwenza Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ambaye ni mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka hapa nchini, Amezuiliwa kuendesha event yake ya ‘Zari All White Party’ hapa nchini Tanzania na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kile kinachosemekana kwamba hakutimiza masharti aliyowekewa kabla ya kufanya event hiyo mara ya mwisho kufanyika hapa Dar es salaam.

Zari alianza kufanya matangazo ya event yake kabla ya hajakamilisha taratibu zote za BASATA mnamo mwaka 2014, na kwa kosa hilo alipewa faini ya kiasi cha fedha TZS 460,000/- na kuzuiliwa kufanya event hiyo hapa nchini mpaka atakaporuhusiwa, na hiyo ni endapo atafata kanuni na taratibu zote alizowekewa na Baraza la Sanaa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts