Home » » Fid Q kuandaa Script ya Wimbo Mpya wa Bella

Fid Q kuandaa Script ya Wimbo Mpya wa Bella

Written By Vuvuzela on Sunday, July 17, 2016 | 3:28:00 PM


Wasanii wengi kwa sasa wanashindana na soko la muziki ili kuhakikisha wanapenya kimataifa na kuweza kuutangaza vyema muziki wa tanzania na ndio sababu ya kupanda ndege kwenda kutafuta mandhari pamoja na video kali.

Mfalme wa sauti bongo kama anavyojiita Christian Bella ameweka wazi suala lake la kwenda nchini Afrika Kusini kufanyia video wimbo wake mpya utakao kwenda kwa jina la Nishike huku msanii wa mashairi ya hip hop  Fid Q akiwa muandaaji wa script.

"nimekaa muda mrefu bila kuachia wimbo, sasa nitaenda na bw. Farid kwa ajili ya kunichorea script kwani tulipokua sweeden nilimuona akichora script na nikagundua ni muandaaji mzuri”.

Bella amesema pia bado kuna wimbo ambao ameshirikiana na Fid Q na yeye ameimba kiitikio hivyo mashabiki wautarajie  wimbo huo kwani upo karibuni kuachiliwa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts