Home » » Ikulu Yaagiza Wakurugenzi wapya Wafike na Nakala Halisi za Vyeti Kabla Ya Kuapa, kwa ajili ya ukaguzi

Ikulu Yaagiza Wakurugenzi wapya Wafike na Nakala Halisi za Vyeti Kabla Ya Kuapa, kwa ajili ya ukaguzi

Written By Bigie on Sunday, July 10, 2016 | 9:00:00 AM

 
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi anapenda kuwataarifa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya walioteuliwa tarehe 07 Julai, 2016 kuwa watakapofika Ikulu Dar es salaam kwa ajili ya kula kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 wahakikishe wanakuja na nakala zao halisi za vyeti vya kitaaluma (Original Academic Certificates).
 
Ieleweke kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma (Original Academic Certificates) unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi (Photocopies).
 
Uhakiki huu wa vyeti utaanza saa mbili asubuhi na wahusika wote mnaombwa kuingia Ikulu kwa kupitia geti kuu la lililopo upande wa mashariki (Upande wa Baharini)
Tafadhali zingatia maelekezo haya.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
09 Julai, 2016

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts