Home » » Jux asema "Kama hakuna wivu basi hakuna mapenzi"

Jux asema "Kama hakuna wivu basi hakuna mapenzi"

Written By Vuvuzela on Monday, July 25, 2016 | 10:31:00 PM


Msanii Jux ambaye sasa ni mpenzi wa Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa wimbo wake mpya 'Wivu' ambao unafanya vizuri kwa sasa hajaimba kwa ajili ya mpenzi wake Vanessa Mdee.
Ameimba wimbo huo kutokana na hisia kwani jambo hilo linawakuta wengi ambao wanapendana kweli katika mahusiano yao ya kila siku.

Jux alidai kwenye mapenzi kama hakuna wivu kati ya wawili wapendanao hapo kunakuwa hakuna mapenzi ya kweli kati yao kwani wivu ndiyo ishara ya upendo wa kweli.


"Wimbo wa Wivu ni matukio ya kimapenzi ambayo yanatokea kwa watu wengi ila siyo kama nimejiimbia mimi, unajua kabla sijarekodi wimbo ule tukiwa studio niliwauliza wakina Bob Manecky na wengine jamanii mnadhani 'idea' hii inaweza kuwa sawa ndipo hapo wakaniambia ni wazo zuri kwani kwenye mapenzi bila uwepo wa wivu kuna kuwa hakuna mapenzi ya kweli, ndiyo hapo nikajua kumbe suala hili linawagusa watu wengi" alisema Jux.


Mbali na hilo Jux amesema kuwa hivi sasa muzuki unakuwa kama haupo kutokana na ukweli kwamba watu wanatanguliza life style mbele kuliko hata kazi zao na ndiyo maana wasanii wengi wakitaka kutoa kazi zao wanafanya mambo mbalimbali kutafuta kiki ili waweze kutambulisha kazi zao hizo.


"Sipendi sana kuulizwa maswali juu ya Vanessa napenda niulizwe maswali juu ya kazi zangu mimi kama msanii, ili nitangaze kazi zangu mimi ndiyo maana kuna vitu saizi sisi tunavikwepa kwa makusudi, tunataka kurudisha muziki hivyo mambo ya kiki, life style tunataka yakae pembeni" alisema Jux

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts