Home » » Kala Jeremiah afichua maajabu ya mtoto huyu aliyemshirikisha ‘Wana Ndoto’

Kala Jeremiah afichua maajabu ya mtoto huyu aliyemshirikisha ‘Wana Ndoto’

Written By Vuvuzela on Thursday, July 21, 2016 | 8:50:00 AM


Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah anaendelea na nyimbo zake za kiuwanaharakati ambapo anatarajia kuachia wimbo wake mpya ‘Wana Ndoto’ aliomshirikisha binti mdogo.

Rapper huyo alisema wimbo huo unazungumzia maisha ya jamii pamoja na watoto wadogo ambao wanandozo za kufanya mambo fulani katika maisha yao.

Jumatano hii, Kala ameamua kuweka wazi uwezo na binti huyo ambaye amemshirikisha katika wimbo huo.“Nimewahi kukutana na watoto wengi wenye vipaji lakini sijawahi kukutana na mtoto mwenye kipaji cha hali ya juu kama huyu mtoto,” aliandika Kala kupitia instagram.

Aliongeza, “Anauwezo mkubwa sana wa kuimba na ana akili nyingi sana. Mungu kambariki sana. Ukitaka kuamini hayo subiri tarehe 26/7 /2016 siku ambayo ‪#‎wanandoto‬ inatoka. huyu ndiye kaimba kiitikio. wakati unaendelea kusubiri Wana Ndoto unaweza kwenda youtube na kuandika miriam chirwa utaona mambo yake. na utaamini ninachokisema,”

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts