Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (Nemc), limekitoza faini
ya Sh15 milioni Kiwanda cha Saruji cha Dangote kwa kosa la kuwapo kwa
taka ngumu na kukosekana kwa choo cha wateja wao na kulazimika
kujisaidia porini.
Hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina
kutembelea kiwanda hicho na kushuhudia shughuli zinazofanyika.
Mratibu
wa Nemc Kanda ya Kusini, Lewis Nzila alisema kutokana na kiwanda hicho
kukiuka sheria za mazingira wanalazimika kulipa faini hiyo ndani ya siku
saba na kujenga choo cha muda ndani ya wiki mbili na kutengeneza
maegesho ya magari ya mizigo ili kuepukana na vumbi.
Awali, Mpina alitaka vyoo vya muda vijengwe ndani ya siku 14 na kulipa faini ndani ya siku saba.Mkuu wa Idara ya rasilimali Watu kiwandani hapo, Kajele James alisema watatekeleza maagizo yote yaliyotolewa.
Post your Comment