Home » » Malecela Aunga mkono kasi ya Rais Magufuli

Malecela Aunga mkono kasi ya Rais Magufuli

Written By Vuvuzela on Friday, July 22, 2016 | 8:33:00 AM


Makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, Dk John Malecela amemsihi Rais John Magufuli kuendelea na kasi yake na kutaka asibadilike hata kama akipewa uenyekiti wa chama hicho.

Alisema hayo wakati akizungumza kwa muda mfupi na waandishi wa habari wakati akikabidhi madawati 127 aliyochangia na marafiki zake kwa mkuu wa wilaya ya Chamwino, Dodoma.

Dk Malecela aliyewahi kuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais, alisema kasi ya Rais Magufuli isiishie katika serikali tu, bali iingie hadi katika chama.

“Nakubaliana na utaratibu mzima wa kumkabidhi kijiti Rais Magufuli, lakini nataka akiingia aendeleze kasi hiyo ili amulike na kuwaondoa wasiofaa kwenye chama”, alisema.

Baada ya kusema hayo alisema anaiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa kutaka kuhakikisha kila mwanafunzi anaketi kwenye dawati na kuwaasa walimu kuangalia utunzaji wa madawati hayo.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts