Home » » Mazungumzo na Masuluhisho wa mgogoro wa Burundi Kuanza Tena Julai 12, Mkoani Arusha

Mazungumzo na Masuluhisho wa mgogoro wa Burundi Kuanza Tena Julai 12, Mkoani Arusha

Written By Bigie on Monday, July 11, 2016 | 10:20:00 AM


Duru ya pili ya mazungumzo kusaka maridhiano nchini Burundi yanatarajiwa kuanza Jumanne Julai 12 hadi Julai 14, 2016.

Taarifa iliyotolewa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, imesema mazungumzo hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha, AICC, chini ya muwezeshaji wake, Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.

Tayari Mh. Mkapa amekwishakutana na Marais wastaafu wa Burundi, viongozi wa vyama vya siasa, dini, mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na kufanya mashauriano na masuluhisho wa mgogoro wa Burundi, Rais Yoweri Museveni wa Uganda .

Katika mazungumzo yake na wadau hao, masuala muhimu kadhaa yaliibuka ikiwemo utekelezaji wa makubaliano ya Arusha ya amani na maridhiano ya Burundi, Katiba ya Burundi, hali ya usalama, nafasi ya siasa na demokrasia, hali ya uchumi na pia mchango wa nchi wanachama wa EAC na nchi nyingine jirani katika mazungumzo hayo. 

Hivyo, duru ya pili ya mazungumzo itajikita zaidi katika kufikia makubaliano ya pamoja kwa ajili ya kuleta utengamano, maendeleo na mustakabal wa Burundi.
 

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts