Home » » Meneja wa Young Dee Afunguka ya Moyoni kuhusu mabadiliko ya Young Dee

Meneja wa Young Dee Afunguka ya Moyoni kuhusu mabadiliko ya Young Dee

Written By Bigie on Monday, July 11, 2016 | 11:35:00 AM


Mkurugenzi wa label ya ‘MDB’ ambayo inamsimia rapper huyo, Max Rioba, kupitia instagram yake ameandika haya kuhusu rapper huyo.

“Namwomba Maulana akusimamie mwanangu uendelee kufanya vizuri na uishangaze dunia na walimwengu wakaao ndani yake. Shikilia hapo hapo uliposhikilia, utafanikiwa tu,” alisema Max.

“Muamini Mungu, muombe yeye akupe ujasiri wa kuushinda moyo kila unapohisi unakaribia kuanguka. Akupe akili za utambuzi uone kisiki kilichoko mbele yako kabla hujajikwaa. Awabariki wale wote wanaochukia maamuzi yako na kuwabariki zaidi wanaokuunga mkono, nayaandika haya kutoka moyoni mwangu Dee. Naamini una nyota inayoweza kung’aa hadi mbali sana,”

Aliongeza, “Najua wako watu wengi sana wanaochukia sana hii movement, Lakini kamwe usiwasikilize. Uliamua mwenyewe kuanguka, ukaamua mwenyewe kuamka. Amua mwenyewe kushikilia msimamo wa mabadiliko yako. Kuna kijana mwingine anaepitia mambo kama uliyoyapitia anasubiri aone umesimama imara naye apate nguvu za kunyanyuka. Fight for yourself, work it out, force your damn self to stay up tight, to stay on top. Then uone utakavyofanikiwa. You’re not a star Dee, you’re a megastar, bigger than a superstar!!! Hands Up y’all. I’m done,”..

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts