Home » » Meya wa Kinondoni Awaachisha kazi Watumishi wanne,na wengine kupewa Onyo kali

Meya wa Kinondoni Awaachisha kazi Watumishi wanne,na wengine kupewa Onyo kali

Written By Vuvuzela on Friday, July 29, 2016 | 9:34:00 AM

Baraza la madiwani chini ya meya wa manispaa ya Kinondoni Jacob Steven limewachukulia hatua watumishi 18 waliokuwa na tuhuma mbalimbali, watumishi 9 wa uhandisi, 8 afya na 1 wa utumishi fedha na biashara,
Watumishi wa 4 afya wamefukuzwa kazi kwa utoro na rushwa, watumishi 3 uhandisi wamekutwa na hatia kwa kushushwa vyeo na madaraja na mtumishi wa fedha na biashara amepewa onyo kali.

Uamuzi huo kwa wahandisi umetokana na wao kushindwa kutumia taaluma zao vizuri kwenye ujenzi wa barabara.Watumishi hao walichukuliwa hatua baada ya kufunguliwa mashtaka, kufanyiwa uchunguzi wa tuhuma zao na wao kupewa muda wa kujitetea.

Baraza la madiwani limewapandisha vyeo watumishi 372, kuwabadilisha vyeo watumishi 9, na kuwathibitisha kazini watumishi 206 ambao walimaliza vipindi vya majaribio na kuonekana kuwa wanafaa kuwa watumishi wa umma

Nawapa hongera kwa kufanya kazi hii kwa weledi na sio kwa show off, wanaofanya kazi kwa show off ili kuonekana wanafanya kazi na wanapenda haki kumbe wana sura mbili wangeiga mfano huu

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts