Home » » Maridhiano ndiyo lugha ya upinzani- Mbatia

Maridhiano ndiyo lugha ya upinzani- Mbatia

Written By Bigie on Friday, July 8, 2016 | 10:44:00 AM


Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Injinia James Fransis Mbatia amesema kwamba maamuzi yoyote ambayo kambi ya upinzani itayafanya endapo wataitwa na kamati ya maridhiano juu ya kususia Bunge wao watakachoangalia ni maslahi ya kitaifa.

Injinia Mbatia ameyasema hayo kuhusu hoja ya wao kukutanishwa na kamati ya maridhiano kujadili kitendo chao cha kususia bunge la bajeti.

''Sisi kabla ya kufanya jambo lolote tunaangalia mama Tanzania kwanza, swala la maridhiano limekuwa jambo letu mara zote , tangu tumeanza masuala ya katiba pamoja na mambo ya demokrasia tuna'' amesema Mbatia.

''Sisi hatujadili mtu tunajadili mfumo, Bunge kwa mujibu wa katiba linatakiwa lisimamie serikali na kuishauri kwa kuheshimu utu na kuhakikisha yale tunayoyafanya yanakuwa na maslahi ya taifa'', Amesema Mbatia.

Mgogoro wetu na Naibu Spika ni kwamba anaongoza Bunge kwa kuagizwa na serikali na hii itaonekana wazi kwamba hoja ya maslahi ya wabunge wabunge wa CCM waliosema hapana walikuwa ni wengi na walikuwa wao kwa wao lakini akasema anatumia kura ya veto hivyo hoja hiyo imepita.

Mbatia amehitimisha kwa kusema watanzania wategemee kama hali ya maridhiano haitapatikana wategemee mambo hayohayo ya kususia mambo kurudi kwenye jamii mfano tuu suala la VAT, serikali imeshindwa kulifafanua kwa kuwa waziri amesema la kwake, gavana wa benki akasema la kwake, na mkurugenzi wa TRA akasema la kwake.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts