Home » » Mwakyembe aridhia kufutwa kwa taasisi zaidi ya 600

Mwakyembe aridhia kufutwa kwa taasisi zaidi ya 600

Written By Bigie on Saturday, July 9, 2016 | 10:52:00 AM

Waziri wa Katiba na Sheria nchini Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Serikali kupitia mamlaka ya wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (RITA) inatarajia kuzifutia usajili bodi 500 za udhamiri kutokana na bodi hizo kuacha kufanya kazi zake kiufanisi na kuisababishia serikali hasara ya fedha ambazo zinatumika bila kuwa na faida kwa Watanzania.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na bodi ya Mamlaka ya Rita kwa lengo lakufanya marekebisho mbalimbali sambamba na kuweka sheria maalumu ambayo itaipa uwezo bodi hiyo yakuzifutia usajili bodi zote ambazo zinafanya kazi chini ya kiwango.

Amesema Serikali imedhamiria kuongeza na kudhibiti mapato ya nchi sambamba na kuhakikisha bodi zote zilizosajiliwa na ambazo zinapata ruzuku ya Serikali zifanye kazi yake kama ilivyokusudiwa hasa zile za dini na za kijamii.

angalia video hii hapa chini

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts