Home » » Mwandishi wa Gazeti la Majira Elizabeth Mayemba, Afariki dunia

Mwandishi wa Gazeti la Majira Elizabeth Mayemba, Afariki dunia

Written By Bigie on Sunday, July 10, 2016 | 8:25:00 AM


Mwandishi Mwandamizi wa Habari za michezo na burudani wa gazeti la Majira, Elizabeth Mayemba amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake eneo la Tabata kwa Swai jijini Dar es Salaam.
 
Taaifa za awali zinaeleza kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku Julai 9.2016,ambapo inaelezwa alikuwa akijisikia kizunguzungu,ghafla alianguka chini na ndipo alipopatwa na umauti huo licha  ya kukimbizwa Hospitali.

Aidha, Taarifa kutoka kwa mume wa marehemu, Eliza, Bwana Rogers amebainisha kuwa…, alipigiwa simu saa mbili usiku na kuambiwa Eliza alisikia kizunguzungu ghafla na kuanguka chini, alichukuliwa na kupelekwa hospitali baada muda mtu aliyempeleka Eliza hospital alimpigia tena na kumpa taarifa za Eliza kufariki. 

Taarifa nyingine zitatolewa baada ya  ndugu wa marehemu kukutaana. 

Chanzo chetu kinatoa pole kwa ndugu na jamaa wote popote pale walipo. Ni pigo kubwa katika tasnia ya Habari.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts