Home » » Nuh Mziwanda:siwezi kuingilia bifu la Shilole na video queen wa video ya ‘Jike Shupa’

Nuh Mziwanda:siwezi kuingilia bifu la Shilole na video queen wa video ya ‘Jike Shupa’

Written By Bigie on Wednesday, July 6, 2016 | 8:11:00 AM


Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amesema hawezi kuingilia bifu ambalo limezuka kati ya aliyekuwa mpenzi wake Shilole na video queen wa video yake ya ‘Jike Shupa’ aitwae ‘Zuu’

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya label ya ‘LFLG’, ameiambia ubuyu kuwa kwa sasa hawezi kuingilia ugomvi usiyomuhusu.

“Wale ni wanawake kwa hiyo zile ni tofauti zao, siwezi kuingilia na siwezi kuongea chochote, yule demu mimi nilimlipa pesa yake ya video akafanya, kazi yangu kamaliza masuala yake yanayoendelea kimpango wake,” alisema Nuh.

Aliongeza, “Kwa hiyo siwezi kuingilia na wala sitaki kufuatilia na wala sitaki kujua kwa sababu nimeshamalizana nae. Yale ni maisha yake binafsi siwezi kuingilia,”

Shilole na video queen wa video ya ‘Jike Shupa’ wamekuwa wakitupia vijembe katika mitandao ya kijamii.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts