Home » » Papa Misifa afunguka kuhusu kufukuzwa Kaburu Record

Papa Misifa afunguka kuhusu kufukuzwa Kaburu Record

Written By Vuvuzela on Friday, July 29, 2016 | 11:38:00 AM


Akiongea nasi, Papaa Misifa amefunguka kwa kusema yeye hajafukuzwa kama uongozi wa label hiyo ilivyoripoti.

“Mimi sijafukuzwa kwanza na sina mkataba na mtu yeyote, wao walikuja kuniomba mimi kama Aljazira ili twende nikamsaidie kuipeleka kampuni yake mbele na tulikubaliana makubaliano. Lakini kumbe yule jamaa alikuwa hajajipanga, kipato hana, tarehe moja mwezi wa saba eti anakwambia mbona hakuna pesa, mbona pesa hazipatikani?,” alisema Papa Misifa.

“Sasa unapataje pesa bila matangazo yoyote, bila kazi alafu unasema unataka upate pesa kwa haraka kwa sababu umewekeza pesa. Kwa hiyo nikagundua nilikuwa nafanya biashara na mtu ambaye hajui biashara, kwa sababu mtu hata ukiwa unauza nyanya ndani ya mwezi mmoja huwezi ona mafanikio hayo ambayo anayazungumzia bila hata kufanya matangazo yoyote. Kwa hiyo mimi pale nimeondoka nimerudi Aljazira, naendelea kusaidia vijana mbalimbali,” aliongeza.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts