Home » » Rais Magufuli awaapisha Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP),Ikulu leo

Rais Magufuli awaapisha Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP),Ikulu leo

Written By Vuvuzela on Monday, July 18, 2016 | 4:52:00 PM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya Makamishna hao kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo.Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wasimamie utekelezaji wa Sheria bila woga na kuahidi kuboresha maslahi ya Jeshi la Polisi nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP)  mara baada ya kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akiwaongoza Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) 35 na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) 23 kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma mara baada ya kupandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) wakila Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma mara baada ya kupandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) wakifuatilia kwa Makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi (wa pili kutoka kushoto) Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) kula kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma.Wengine ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kutoka kushoto)akizungumza jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (kushoto) leo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) kula kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma.Wengine kulia ni Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Kulia) na Mhe. Hamad Masauni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo.Kutoka kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju,Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (kushoto), Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama leo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP).Picha/A.Msigwa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts