Home » » Rais Magufuli awaapisha Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Walimu

Rais Magufuli awaapisha Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Walimu

Written By Vuvuzela on Thursday, July 28, 2016 | 7:25:00 AM

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Bw. Oliva Paul Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

Aidha, Rais Magufuli amemuapisha Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu tarehe 15 Julai, 2016.

Viongozi hawa wanakuwa wa kwanza kuongoza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) tangu Tume hiyo ilipoundwa kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Namba 25 ya mwaka 2015 ikiwa na majukumu ya kusimamia na kuratibu masuala yanayohusu utumishi wa walimu.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma

27 Julai, 2016

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts