Get the latest updates from us for free

Home » » Roma Mkatoliki afunguka kuwa ataendelea kuichana Serikali pale inakosea na kuisifia pale inapotenda mambo mema

Roma Mkatoliki afunguka kuwa ataendelea kuichana Serikali pale inakosea na kuisifia pale inapotenda mambo mema

Written By Vuvuzela on Saturday, July 2, 2016 | 10:13:00 AM


Msanii Roma Mkatoliki amefunguka na kusema kuwa ataendelea kuichana Serikali pale ambapo inakosea na wataisifia pale inapotenda mambo mema kwa jamii na amesisitiza kuwa yeye anaamini kuwa mpaka sasa katika uongozi wa Rais Magufuli kuna mambo mengi ya kuzungumza au ya kuimba kwani kuna matukio mengi yaliyotokea ambayo jamii inataka majibu yake.

“Tutaendelea kuichana Serikali pale inapokosea na itasifiwa pale inapofanya mambo ya msingi kwa jamii, ila mpaka sasa kuna mambo mengi ya kuimba kwenye uongozi huu, hata jamii nayo inaposikia nataka kutoa kazi watu wanaanza kujiuliza, mambo kama bunge live, Sukari, hivyo kunamambo mengi sana ya kuimba” alisisitiza Roma Mkatoliki.

Roma Mkatoliki amesema kuanzia sasa muda wowote ataachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Kaa Tayari’ hivyo watu wasubiri kusikia ndani ya wimbo huo ameimba nini.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts