Home » » Shahidi akwamisha Kesi ya IPTL dhidi ya Zitto Kabwe

Shahidi akwamisha Kesi ya IPTL dhidi ya Zitto Kabwe

Written By Bigie on Monday, July 4, 2016 | 10:04:00 PM

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ilifungua kesi ya madai ya fidia ya Sh. bilioni 500  Mahakama kuu, kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Zitto Kabwe. 

IPTL pamoja na wadai wenzake waliiomba mahakama imwamuru Zitto kulipa fidia hiyo kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kimaandishi

Kesi hiyo dhidi ya Zitto Kabwe na gazeti la Raia Mwema leo imeahirishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania mpaka August 24 2016 baada ya mawakili wa IPTL kusema shahidi wao muhimu ameumwa ghafla hivyo hataweza kutoa ushahidi.

Katika kesi hiyo IPTL na mmiliki wake wanadai walipwe Tshs 500,000,000 (Bilioni mia tano) kwa madai kwamba gazeti la Raia Mwema liliandika uongo dhidi ya IPTL kuhusu hela zilizoibiwa kwenye Escrow Akaunti.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts