Home » » Ukali wa Rais Magufuli kwenye ukusanyaji Kodi wasababisha Mafuriko TRA

Ukali wa Rais Magufuli kwenye ukusanyaji Kodi wasababisha Mafuriko TRA

Written By Bigie on Tuesday, July 5, 2016 | 6:42:00 PM


Tangu aingie madarakani Novemba 5 mwaka jana, Rais wa Awamu ya Tano Magufuli amekuwa akisisitiza ulipaji kodi hali ambayo imesababisha mapato kwa mwezi kuongezeka kutoka wastani wa Sh. bilioni 800 mpaka Sh. trilioni 1 kwa mwezi.

Rais Magufuli ameanzisha pamoja na nyingine, kampeni ya kudai risiti pindi mwananchi anaponunua bidhaa yoyote.Chanzo chetu kilizunguka katika ofisi za Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni na Ilala jana na kukuta misusuru ya watu wanaotaka kukata leseni za biashara.

Ofisa habari wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera alisema idadi ya wafanyabiashara wanaofika kulipia leseni ya biashara imeongezeka katika halmashauri hiyo kutokana na sababu kadhaa, ikiwamo wafanyabiashara kuogopa kupigwa faini kutoka na kuanza kwa mwaka mpya wa serikali.

Lakini, alisema, wafanyabiashara wengi pia walikuwa wanafanya biashara zao kwa kuiibia serikali kwa kutokulipa kodi, na kwamba "kuingia kwa serikali ya awamu ya tano kumesaidia kuwaamsha wafanyabiashara hao." “Kujua tumeshapata kiasi gani, inakuwa ni ngumu kwa sababu wanalipia katika benki, hivyo ni hadi nifuatilie ngazi za juu kujua makusanyo lakini kila siku watu wanalipa,” alisema Mhowera.

Hali ya misururu ilikuwapo pia katika ofisi za TRA jijini jana ambapo wananchi walikuwa wakichukua namba za TIN kwa dhumuni la kwenda kupata leseni za biashara katika Halmashauri za Kinondoni, Ilala na Temeke.
Wengine, pia, walikuwa wakiwasilisha risiti za malipo ya kodi mbalimbali.

Akizungumza Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alithibitisha kuwa kuna ongezeko la wafanyabiashara wanaofika katika ofisi za TRA kuchukua TIN kwa lengo la kwenda kukata leseni. Alisema ongezeko la watu hao ni tofauti na miaka ya nyuma. “Idadi (ya watu kwenye Ofisi za TRA) ni kubwa kweli, (lakini) hata ukipita katika ofisi zetu zilizopo katika wilaya utakuta kuna watu wengi wakichukua TIN namba kwa ajili ya kufungua biashara zao, mwitikio ni mkubwa tofauti na miaka ya nyuma,” alisema Kayombo.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts