Home » » Wadaiwa sugu wa HESLB waanza kujitokeza

Wadaiwa sugu wa HESLB waanza kujitokeza

Written By Vuvuzela on Sunday, July 31, 2016 | 11:20:00 AM


Hivi karibuni Bodi ya Mikopo imesema itawachukulia hatua wale wote ambao hawatalipa madeni yao ikiwemo kufikishwa mahakamani, kutozwa faini,kunyimwa fursa za kupata mikopo, kunyimwa fursa za masomo nje ya nchi na kuzuiwa kusafiri nje ya nchi.

Akizungumza nasi jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa alisema tangu waanike majina ya wadaiwa sugu kumekuwa na shauku ya watu wengi kufuatilia taarifa zao za fedha walizokopa wakati wanasoma.

Alisema kutokana na muamko huo ndio maana wameamua kuongeza siku za kufanyakazi hadi Jumapili ili kuwawezesha wadaiwa hao kupata taarifa na kwenda kulipa madeni wanayodaiwa.

Aidha, Mwaisobwa alisema wapo baadhi yao wameanza kulipa madeni yao, lakini hadi sasa kiwango cha fedha zilizolipwa haijafahamika kwa kuwa wahasibu wanafanya mahesabu yao kila mwisho wa mwezi na kutolewa ripoti.

“Sio rahisi kujua kiwango cha fedha zilizokusanywa kwa kuwa kila mmoja anaenda kulipia benki na wahasibu wetu kila mwisho wa mwezi hufanya mahesabu yao na kutupatia ripoti,” alisema Mwaisobwa.

Mwaisobwa alisema mwanafunzi ambaye amemaliza chuo kikuu anatakiwa kuanza kulipa deni lake baada ya kipindi cha mwaka mmoja.

”Kwa yule ambaye ameacha chuo ama kufukuzwa anatakiwa kuanza kulipa deni lake katika kipindi hicho bila ya kuongezewa deni na kwa yule ambaye anachelewa kulipa kila mwaka anapata penati ya asilimia tano ya deni analodaiwa,” alisema.

Aidha alisema kwa mwanafunzi ambaye ataomba chuo ama kuhama chuo anatakiwa kutoa taarifa kwa Bodi ya Mikopo ili kuepusha ubadhirifu wa fedha kwa baadhi ya chuo.

“Inapotokea umeacha chuo halafu umeomba mkopo ina maana fedha yako uliyoomba itapelekwa kwenye chuo ulichoacha na sisi lazima tukudai maana tunajua wewe umepokea hizo hela kwa kuwa hujatupatia taarifa ya kuacha chuo hivyo ni vizuri kutoa taarifa kwa bodi ya mikopo, chuo kisipokuwa na waaminifu wanazitumia hizo fedha zako,” alisema

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts