Home » » Watu 11 mbaroni kwa madawa ya kulevya Mkoani Ruvuma

Watu 11 mbaroni kwa madawa ya kulevya Mkoani Ruvuma

Written By Bigie on Saturday, July 9, 2016 | 9:35:00 AM

 
Watu tisa wanakishikiliwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kukutwa wakifanya biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi kilo 96 na kete 176 huku wengine wawili wakikamatwa na pombe haramu ya gongo lita 67.
 
Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Zuberi Mwombeji (pichani) aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Gabriel Ndabaliuze (37), mkazi wa Bombambili, Evance Mkonde (24), mkazi wa Lizaboni na Gwaita Shaib (35), mkazi wa Namanditi ambao kwa pamoja walikamatwa na bangi kilo 34 maeneo ya Matarawe, Songea Mjini.

Kamanda Mwombeji alisema kuwa watuhumiwa wengine, Costa Mwinuka (49), mkazi wa Mkuzo, Angeleus Hyera (39), mkazi wa Lupapila na Zamtanga Gama (42), mkazi wa Mjimwema walikutwa eneo la Sido, Songea wakiwa na bangi kilo 41.

Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Felician Mgaya (44), Mustapha Rashid na Mrisho Mponda (19), wakazi wa Hoahoa Mbinga, ambao walikamatwa na bangi kilo 7 na kete 132 na Hija Omari Hashimu, mkazi wa Nakapanya, Tunduru aliyekamatwa na bangi kilo 5.

Kamanda huyo aliongeza kuwa watuhumiwa wengine, Hassan Mtulule (32) na Twalib Abbas (30) wakazi wa Tunduru walikamatwa na pombe haramu ya gongo lita 67 na kwamba upelelezi unaendelea na mara utakapokamilika, watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts